Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekutana na wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Zaidi ya watu walihudhuria mkutano huo ambapo hata serikali iliwapangia usafiri kutoka makwao.Rais Jonathan amekosolewa sana kuwekewa shinikizo aongeze kasi katika jitihada za kuokoa wasichana hao waliotekwa nyara siku miamoja zilizopita.
Wazazi hao walijiondoa katika mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika kati yao na Rais Jonathan wiki jana wakisema kuwa wanahitaji mwazo kushauriana na familia zengine za wale ambao watoto wao walitekwa.
Rais Jonathan amesema kuwa wazazi hao walichochewa na wanaharakati ambao aliwatuhumu kwa kuingiza siasa katika swala hilo zima.
Maafisa wanasema zaidi ya watu 40 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Boko Haram mjini humo Ijumaa.
Wapiganaji hao pia walishambulia vijiji vingine sita.
Kadhalika wapiganaji hao wamefanya mashambulizi mengine mjini Damboa ambako waliharibu milingoti na nyaya za stima na kuwaacha wakazi wa jimbo la Borno bila umeme kwa wiki kadhaa zilizopita.
No comments:
Post a Comment