Ni ukweli unaohitaji kujulikana na kila mtu! Ukweli huuni kwamba, mtu aliumbwa na Mungu katika maeneo mawili kwa wakati mmoja! Maeneo haya mawili ni ulimwengu wa roho na ulimwengu wa kimwili!
Unaposoma mistari kadhaa katika biblia, unaona ya kuwa mtu aliumbwa na Mungu, kwa namna ambavyo, anaweza kuishi kwa wakati mmoja katika ULIMWENGU WA ROHO na ULIMWENGU WA KIMWILI PIA.
Maneno ya 1 WATHESALONIKE 5:23 yanatuambia hivi: "MUNGU WA AMANI MWENYEWE AWATAKASE KABISA; NANYI NAFSI ZENU NA ROHO ZENU NA MIILI YENU MHIFADHIWE MWE KAMILI, BILA LAWAMA, WAKATI WA KUJA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTO". Kwa hiyo mtu ni nafsi, roho na mwili kwa pamoja!
Lakini ukiendelea kuisoma mistari mbalimbali katika Biblia utaona ya kuwa, vitu hivi vitatu vimeumbwa na kuwekwa kwa mpangilio maalum. Utaona MTU NI ROHO, ANAYO NAFSI, NA ANAKAA KATIKA MWILI!.
Na Mungu amemuumba mtu kwa namna ambayo, roho ya mtu inatakiwa imiliki nafsi yake na imiliki mwili wake pia! Ndiyo maana unamsoma Mtume Paulo akisema "MWILI WANGU" na akisema; "NAFSI YANGU" (WARUMI 7:18,20).
Mtu ameumbwa ili aishi na awe na nafasi katika ulimwengu wa roho na katika ulimwengu wa kimwili pia; kwa roho aishi katika ulimwengu wa roho, na kwa mwili wake aishi katika ulimwengu wa kimwili.
Tena, kwa nafasi yake awasiliane na awe na mahusiano kati ya roho na mwili wake; au awe na mahusiano yenye maelewano kati ya ulimwengu wa kirohi na ule ulimwengu wa kimwili. Jukumu kubwa la nafasi ni like la kuwa mtafasiri kati ya roho ya mtu husika na mwili wake!
Hili ni muhimu, kwa kuwa lugha ya ulimwengu wa roho ni tofauti na ile lugha ya ulimwengu wa kimwili; kwa hiyo roho na mwili havielewani bila mtafsiri katikati yao! Ndiyo maana tunasoma ya kuwa; " WALE WAUFUATAO MWILI HUYAFIKIRI MAMBO YA MWILI: BALI WALE WAIFUATAO ROHO HUYAFIKIRI MAMBO YA ROHO" ( WARUMI 8:5).
No comments:
Post a Comment