Makubaliano ya kusitisha
mapigano katika eneo ilipoanguka ndege ya Malaysia wiki iliyopita,
yamefikiwa na pande zote kinzani , serikali ya Ukraine na wanamgambo
wanaounga mkono Urusi.
Treni iliyobeba miili ya waliofariki katika
mkasa huo wa ndege imewasili mjini Kharkhiv, mji unaodhibitiwa na
serikali ya Ukraine, ikiwani ni siku 5 tangu kudunguliwa kwa ndege hiyo.Wanamgambo hao pia wamewakabidhi wachunguzi Vifaa vya rekodi mwenendo wa ndege hiyo- viitwavyo blackbox .
Uchunguzi wa kina unahitaji kufanywa kubaini nani hasa alihusika na undunguliwaji wa ndege hiyo.
Utawala wa Ukrain na nchi za magharibi zinadai wanamambo walisaidiwa na Urusi kuidungua ndege hiyo.
Wachunguzi wa kimataifa wameruhusiwa kuingia katika eneo la ajali baada ya baraza la usalama la UN kupitisha azimio.
Mwanachama mmoja wa kikundi cha wachunguzi, alisema kuwa wameweza kukata vipande vya mabaki ya ndege na kwamba kwa sasa wako katika eneo hilo.
Wanamgambo hao na Urusi wanakana vikali madai hayo.
Ndege hiyo ilianguka Alhamisi iliyopita na kuwaua watu 298.
No comments:
Post a Comment