Hoja ya hali ya kiakili ya Pistorius
Upande wa mashitaka katika kesi
dhidi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius umetoa ombi la
kutaka mwanariadha huyo kufanyiwa uchunguzi wa kiakili wakati kesi hiyo
ikiendelea.
Wakili Gerrie Nel aliwasilisha ombio hilo kwa
mahakama baada ya mtaalamu wa matibabu ya kiakili Merryll Vorster kusema
kuwa Pistorius ni hatari kwa jamii.Pistorius amekana madai ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka jana. Alisema kuwa alimpiga risasi kwa bahati mbaya akidhani kuwa alikuwa jambzi aliyekuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka unatuhumu upande wa utetezi kwa kubadilisha kauli yake mwanzo kwa kusema kuwa Pistorius alilamizimika kufyatua risasi baada ya kuhofia usalama wake na sasa anasema kuwa alikuwa na tatizo la kiakili.
Bwana Nel alisema kwamba uchunguzi huo ni muhimu hasa kwa sababu ya kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa hivyo ni sawa kwa Pistorius kwenda kuchunguzwa.
Daktari, Vorster aliambia mahakama kwamba hasemi kuwa Pistorius ana tatizo la kiakili na kwamba bado anaweza kutenda vyema kazi yake ya riadha na pia bado ana uwezo wa kuwasiliana na watu wengine vyema tu.
Lakini alisema kuwa watu wenye tatizo la kuwa na wasiwasi wakati wote kama Pistorius hawapaswi kuruhusiwa kujihami.
No comments:
Post a Comment