Sunday, September 20, 2015

ULIMUBWA ILI UISHI MAENEO MAWILI KWA WAKATI MMOJA.

Ni ukweli unaohitaji kujulikana na kila mtu! Ukweli huuni kwamba, mtu aliumbwa na Mungu katika maeneo mawili kwa wakati mmoja! Maeneo haya mawili ni ulimwengu wa roho na ulimwengu wa kimwili!
Unaposoma mistari kadhaa katika biblia, unaona ya kuwa mtu aliumbwa na Mungu, kwa namna ambavyo, anaweza kuishi kwa wakati mmoja katika ULIMWENGU WA ROHO na ULIMWENGU WA KIMWILI PIA.
Maneno ya 1 WATHESALONIKE 5:23 yanatuambia hivi: "MUNGU WA AMANI MWENYEWE AWATAKASE KABISA; NANYI NAFSI ZENU NA ROHO ZENU NA MIILI YENU MHIFADHIWE MWE KAMILI, BILA LAWAMA, WAKATI WA KUJA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTO". Kwa hiyo mtu ni nafsi, roho na mwili kwa pamoja!
Lakini ukiendelea kuisoma mistari mbalimbali katika Biblia utaona ya kuwa, vitu hivi vitatu vimeumbwa na kuwekwa kwa mpangilio maalum. Utaona MTU NI ROHO, ANAYO NAFSI, NA ANAKAA KATIKA MWILI!.
Na Mungu amemuumba mtu kwa namna ambayo, roho ya mtu inatakiwa imiliki nafsi yake na imiliki mwili wake pia! Ndiyo maana unamsoma Mtume Paulo akisema "MWILI WANGU" na akisema; "NAFSI YANGU" (WARUMI 7:18,20).
Mtu ameumbwa ili aishi na awe na nafasi katika ulimwengu wa roho na katika ulimwengu wa kimwili pia; kwa roho aishi katika ulimwengu wa roho, na kwa mwili wake aishi katika ulimwengu wa kimwili.
Tena, kwa nafasi yake awasiliane na awe na mahusiano kati ya roho na mwili wake; au awe na mahusiano yenye maelewano kati ya ulimwengu wa kirohi na ule ulimwengu wa kimwili. Jukumu kubwa la nafasi ni like la kuwa mtafasiri kati ya roho ya mtu husika na mwili wake!
Hili ni muhimu, kwa kuwa lugha ya ulimwengu wa roho ni tofauti na ile lugha ya ulimwengu wa kimwili; kwa hiyo roho na mwili havielewani bila mtafsiri katikati yao! Ndiyo maana tunasoma ya kuwa; " WALE WAUFUATAO MWILI HUYAFIKIRI MAMBO YA MWILI: BALI WALE WAIFUATAO ROHO HUYAFIKIRI MAMBO YA ROHO"  ( WARUMI 8:5).

Tuesday, July 22, 2014

Hatimaye Rais Goodluck akutana na wazazi


Baadhi ya wazazi ambao watoto wao walitekwa nyara

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekutana na wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Zaidi ya watu walihudhuria mkutano huo ambapo hata serikali iliwapangia usafiri kutoka makwao.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais kukutana na wazazi hao tangu wasichana kutekwa nyara.
Rais Jonathan amekosolewa sana kuwekewa shinikizo aongeze kasi katika jitihada za kuokoa wasichana hao waliotekwa nyara siku miamoja zilizopita.
Wazazi hao walijiondoa katika mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika kati yao na Rais Jonathan wiki jana wakisema kuwa wanahitaji mwazo kushauriana na familia zengine za wale ambao watoto wao walitekwa.
Rais Jonathan amesema kuwa wazazi hao walichochewa na wanaharakati ambao aliwatuhumu kwa kuingiza siasa katika swala hilo zima.
Baadhi wanamkosoa Rais Goodluck kwa kukosa kukutana na wazazi hao hadi aliposhinikizwa na Malala
Wakati hayo yakijiri watu 15,000 wametoroka makwao kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mji wa Damboa baada ya ghasia zinazosababishwa na Boko Haram kukithiri.
Maafisa wanasema zaidi ya watu 40 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Boko Haram mjini humo Ijumaa.
Wapiganaji hao pia walishambulia vijiji vingine sita.
Kadhalika wapiganaji hao wamefanya mashambulizi mengine mjini Damboa ambako waliharibu milingoti na nyaya za stima na kuwaacha wakazi wa jimbo la Borno bila umeme kwa wiki kadhaa zilizopita.

WACHUNGUZI WAANZA KAZI UKRAINE



Treni yenye mabaki ya waathiriwa wa mkasa wa ndege ya Malysia nchini Ukraine
Makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo ilipoanguka ndege ya Malaysia wiki iliyopita, yamefikiwa na pande zote kinzani , serikali ya Ukraine na wanamgambo wanaounga mkono Urusi.
Treni iliyobeba miili ya waliofariki katika mkasa huo wa ndege imewasili mjini Kharkhiv, mji unaodhibitiwa na serikali ya Ukraine, ikiwani ni siku 5 tangu kudunguliwa kwa ndege hiyo.
Kuhamishwa kwa masalia hayo ya ndege iliyoanguka MH17 inakuja baada ya shinikizo kali dhidi ya wapiganaji huku kukiwa na madai kuwa wao ndio walioindungua ndege hiyo.
Wanamgambo hao pia wamewakabidhi wachunguzi Vifaa vya rekodi mwenendo wa ndege hiyo- viitwavyo blackbox .
Mabaki ya ndege iliyoanguka

Uchunguzi wa kina unahitaji kufanywa kubaini nani hasa alihusika na undunguliwaji wa ndege hiyo.
Utawala wa Ukrain na nchi za magharibi zinadai wanamambo walisaidiwa na Urusi kuidungua ndege hiyo.
Wachunguzi wa kimataifa wameruhusiwa kuingia katika eneo la ajali baada ya baraza la usalama la UN kupitisha azimio.
Mwanachama mmoja wa kikundi cha wachunguzi, alisema kuwa wameweza kukata vipande vya mabaki ya ndege na kwamba kwa sasa wako katika eneo hilo.
Wanamgambo hao na Urusi wanakana vikali madai hayo.
Ndege hiyo ilianguka Alhamisi iliyopita na kuwaua watu 298.

Friday, June 13, 2014

Watu zaidi ya 30 wauwawa mashariki mwa Kongo

Watu wapatao 37 wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa mkoani Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumamosi (07.06.2014) katika shambulizi ambalo maafisa wanasema limesababishwa na mzozo wa mifugo.
Wahanga, wakiwemo wanawake wajawazito, walikuwa wamepigwa risasi, kudungwa visu au kuchomwa moto ndani ya nyumba zao. Mpigapicha wa shirika la habari la Reuters katika eneo la tukio katika kijiji cha Mutarule alihesabu maiti 37, baadhi zikiwa zimezagaa ndani ya kanisa la kijiji hicho, kinachopatikana kilometa takriban 50 kutoka Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.
Wakaazi na viongozi wa dini wamesema wagonjwa waliokuwa katika kituo cha matibabu walishambuliwa. Mbali na waliouwawa, watu wengine zaidi ya 20 walijeruhiwa, huku 10 kati yao wakiwa katika hali mahututi.
"Ni raia wa Kongo waliofanya mashambulizi haya. Yanahusiana na mzozo juu ya ngo'mbe," amesema gavana wa jimbo la Kivu Kusini, Mercellin Cishambo, wakati alipozungumza na shirika la habari la Reuters. "Tatizo ni kwamba kila mtu katika eneo hili hubeba silaha." Gavana huyo amekadiria idadi ya watu waliouwawa kuwa 27.
Msemaji wa serikali ya Kongo, Lambert Mende, amesema tukio hilo lilikuwa shambulizi la kulipiza kisasi lililofanywa na jamii ya mchunga ng'ombe mmoja aliyeuwawa wakati wa jaribio la kuiba ng'ombe waliomilikiwa na mkulima mwingine. "Kamanda wa jeshi katika eneo hilo ametiwa mbaroni kwa sababu alichukua hatua za taratibu mno. Anazuiliwa na polisi. Maafisa pia wamemkamata kiongozi mmoja wa eneo hilo anayeshukiwa kuratibu mashambulizi hayo," akaongeza kusema Mende. Mende aidha amesema idadi ya watu waliouwawa katika machafuko hayo ni 34.
Shambulizi la pili
Jimbo la Kivu Kusini, eneo la milima lenye utajiri wa madini ikiwemo dhahabu, ni makazi kwa jamii za makabila yaliyoikimbia nchi jirani ya Burundi baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 2005 na vile vile makundi mengi ya waasi, likiwemo kundi linalopigania ukombozi wa Rwanda, FDLR.
FDLR Kämpfer Wapiganaji wa kundi la FDLR

Baadhi ya wanakijiji kutoka kabila la Bafuliru nchini Kongo wamewalaumu waasi kutoka Burundi wa kundi la FNL kwa mashambulizi hayo. Wakaazi wamesema mwezi Agosti mwaka uliopita watu wanane waliuwawa na watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami na silaha katika kijiji hicho. Kaburi lenye misalaba minane ndio ishara inayoonyesha mahala walipozikwa watu hao.
"Mauaji ya kwanza ya kiholela yalitokea, na sasa la pili limetokea na hatujafahamu kilichotokea wakati wa mauaji ya kwanza," mzee wa mtaa Amuri Kikukama ameliambia shirika la habari la Reuters. "Tunashangaa kwa nini mauaji yanapaswa kuendelea huku serikali ikitazama tu."
Mkaazi mwingine wa pili amesema kundi la waasi wenye silaha wana kambi yao yapata kilometa 20 kutoka kijiji hicho cha Mutarule. Wanakikiji wengi walikuwa wakifungasha virago vyao siku ya Jumamosi kuondoka kwenda katika kijiji kingine.
Tume ya MONUSCO yachukua hatua
Tume ya amani ya Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO, ilitoa taarifa Jumamosi jioni ikisema mapigano makali yalikuwa yametokea usiku wa kuamkia jana kati ya jamii ya Bafuliru kwa upande mmoja na jamii za Barundi na Banyamulenge kwa upande mwingine. Wabarundi na Wabanyamulenge ni Watutsi kutoka Burundi ambao wamekuwa wakiishi Kivu Kusini kwa vizazi kadhaa. Kumekuwa na mzozo kati ya Wabafuliru na Wabarundi kuhusiana na mali za masuala ya mila.
Martin Kobler UNO-Mission Kongo Mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler, akiwa na wanajeshi wa tume hiyo Kongo
Martin Kobler, Mkuu wa tume ya MONUSCO, amesema tume hiyo inatuma wanajeshi zaidi kuwalinda raia. "Vitendo hivi vya umwagaji damu havikubaliki na lazima vikome mara moja," akasema Kobler katika taarifa yake. Wanajeshi wa kulinda amani wa tume hiyo wametumwa Mutarule kuwaondoa watu waliojeruhiwa na kuwasaidia maafisa wa eneo hilo na jeshi la Kongo kurejesha utulivu.
Serikali ya Kongo imesema inapanga kuwashambulia waasi kutoka nje ya nchi wanaoendesha shughuli zao mashariki mwa taifa hilo baada ya kushindwa kundi la waasi wa M23 mwishoni mwa mwaka jana.

CAMEROON UWANJANI LEO HUKO BRAZILI



Cameroon kukabiliana na Mexico baadaye leo

Baada ya kushuhudia mechi ya kwanza ya fainali ya kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil,mamilioni ya mashabiki kutoka bara Afrika hii leo watafungua macho na kupaza sauti zao wawakilishi wa kwanza wa Afrika The Indomitable lions wa Cameroon ikitoana kijasho na Mexico katika mechi ya pili ya kundi A.
Timu hizi zimewahi kukutana mara moja pekee kabla ya hii leo.Mexico ilishinda mechi hiyo ya kujipima nguvu kwa bao moja kwa nunge.
Mechi hiyo ilichezwa huko L.Angeles Marekani mwaka wa 1993 ,lakini hii leo hii haitategemea historia wala ukweli kuwa Mexico haijawahji kuishinda timu yeyote ya Afrika katika kombe la dunia ,la dakika tisini katika uwanja wa Arena das Dunas,ulioko Natal ndizo zitakazoamua yupi kati yao ni kidedea.
Kocha wa Mexico Miguel Herrera atakuwa bila ya mshambulizi nyota Javier Hernandez kutokana na kuwa hajafunga bao lolote katika mechi tisa.
Kocha huyo atawategemea Giovani dos Santos na Oribe Peralta katika safu ya ushambulizi huku akitarajia Guillermo Ochoa kulinda lango lake.
Kwa upande wao Cameroon ambao walifanya mgomo wa marupurupu kabla ya kuabiri ndege ya Brazil ,nyota wao Samuel Etoo anatarajiwa kuanza katika mechi hii licha ya kuwa hayuko timamu kiafya.
The indomitable Lions walifuzu kwa mashindano haya baada ya FIFA kubatilisha matokeo ya kichapo mikononi mwa Togo.
Kocha Volker Finke anakabiliwa na changamoto ya mshikamano wa timu yake iliyowasili Brazil siku nne tu zilizopita baada ya mgomo huo wa marupurupu.
Timu yake ndiyo yenye kushikilia rekodi ya kushindwa mara nyingi kuliko timu zote.
Cameroon imepoteza mechi 24 na kushinda mechi moja pekee kati ya 13 ilizoshiriki.
Cameroon iliilaza Saudi Arabia bao 1-0 mwaka wa 2002.
Katika mashindano haya Camerooon imemshirikisha mchezaji mchanga zaidi katika kikosi chao Fabrice Olinga mwenye umri wa miaka 18.

Uhispania vs Uholanzi
Uhispania vs Uholanzi ni marudio ya fainali ya 2010
Mechi nyengine itakayokuwa ikitazamiwa na mamilioni ya mashabiki kote duniani ni Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania .
Mabingwa hao huko Afrika Kusini mwaka wa 2010 wanafungua kampeini yao dhidi ya Uholanzi katika Arena Fonte Nova, Salvador.
Mechi hii itakuwa kumbukumbu ya fainali miaka minne iliyopita lakini Kocha wa Uhispania Vicente del Bosque hana sababu ya kuwa na wasiwasi kwani anajivunia kikosi dhabiti kinachosheheni mabingwa wa dunia mabingwa wa kombe la Ulaya na mabingwa wa taji la bara Uropa.
kati ya mechi kumi walizochuana Uhispania imeishinda Uholanzi mara tano na ikashindwa mara nne.
Kocha mpya wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal anamtegemea nyota wa united Robin van Persie Wesley Sneijder na Dirk Kuyt kudhibiti tikitaka ya wahispania.
Bila shaka ukitaka kutizama janja na janjaure basi kaa kitako usubiri mechi hii.
Mechi ya mwisho hii leo itakuwa ya baina ya Chile na Australia.
Kinyume na mechi baina ya Uhispania na Uholanzi itakayoshuhudia tiki taka mechi baina ya chile na Australia inatarajiwa kuwa ya kasi na nguvu kutokana na mifumo ya timu hizo mbili.

Chile dhidi ya Australia
CHILE VS AUSTRALIA
Australia haijawahi kushinda mechi yeyote ya kombe la dunia wala alama yeyote ila ile waliojinyakulia mwaka wa 1974 walipotoka sare ya suluhu bin suluhu dhidi ya CHILE
'The Socceroos' wameshindwa na Chile katika mechi zao zote za kujipima nguvu.
Australia ambayo inaorodheshwa katika nafasi ya 62 katika orodha ya timu bora na shirikisho la soka duniani FIFA, ndiyo timu ya chini kabisa katika orodha hiyo ya FIFA inayoshiriki katika mashindano haya huko Brazil.
Kwa upande wao Chile wamewahi kushinda mechi mbili pekee kati ya 17 walizocheza za kombe la dunia.
Chile ilizilaza Honduras na Switzerland huko Afrika kusini mwaka wa 2010.
Wanamtegemea nyota wao Arturo Vidal kuwafungia mabao .
Australia kwa upande wao wanawategemea Mark Bresciano na Tim Cahill kusonga mbele katika hatua ya makundi

Kombe la Dunia laanza rasmi, Brazil yaishinda Croatia


Fainali za kombe la dunia zimefunguliwa rasmi Alhamis(12.06.2014) nchini Brazil, wakati wenyeji Brazil wakipambana na Croatia huko wenyeji wakijaribu kuonesha hisia za tamasha la kanivale.
Weltmeisterschaft Fußball Brasilien 2014 Eröffnungsfeier Sherehe za ufunguzi zilifana

Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi za mipira dhidi ya waandamanaji wanaopinga mashindano hayo mjini Sao Paulo.
Lakini mabingwa hao mara tano wa kombe la dunia Brazil waliwashangaza mashabiki wao baada ya kufungwa goli ambalo limetokana na mchezaji wa Brazil dakika 11 tu tangu kuanza mchezo huo wa ufunguzi katika uwanja wa Corinthians mbele ya mashabiki 61,600 ikiwa ni pamoja na wakuu wa nchi 12.
Straßenszene in Brasilien WM 2014 Barabarani nchini Brazil wakati wa fainali hizi 2014
 
Marcelo akaribia kuangua kilio
Mlinzi Marcelo alikaribia kutiririka machozi baada ya kuusindikiza mpira katika wavu wake kutokana na krosi iliyopigwa na Ivic Olic wa Croatia. Lakini mshambuliaji shujaa wa Brazil Neymar alisawazisha katika dakika ya 29 ya mchezo huo. Brazil ikashinda kwa mabao 3-1.
Polisi wa Brazil walijenga ukuta mduara wa chuma kuzunguka uwanja huo kuwazuwia waandamanaji kusogelea eneo hilo ambalo tamasha hilo kubwa la kandanda litaendelea kwa muda wa wiki nne, ambapo Brazil imetumia kiasi ya dola bilioni 11 kutayarisha.
Weltmeisterschaft Fußball Brasilien 2014 Brasilien vs Kroatien Eigentor Dakika 11 baada ya mchezo kuanza Brazil wanajifunga bao

Lakini waandamanaji waliokuwa na nia ya kuchafua sherehe hizo wakivalia mashati meusi na kujifunika nyuso zao waliwasha moto kwa kutumia takataka , kilometa chache kutoka katika uwanja huo baada ya polisi wenye silaha kujaribu kutuliza ghasia katika saa kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa fainali hizo.
Maandamano yaendelea
Matayarisho ya kombe la dunia yamechafuliwa na miezi kadha ya maandamano, yakiakisi hasira za umma kuhusiana na matumizi ya fedha za maandalizi.
Lakini mji wa Sao Paulo na miji mingine kwa kiasi kikubwa ilikuwa tulivu wakati mchezo ulipoanza. Bendera za rangi ya njano na kijani zilipepea katika majengo mengi.
Weltmeisterschaft Fußball Brasilien 2014 Eröffnungsfeier Polisi wakilinda usalama dhidi ya waandamanaji

Lakini waandamanaji ambao walisababisha vurugu kubwa wakati wa kombe la mabara , Confederations Cup, mwaka jana wameapa kuandamana katika uwanja wa Sao Paulo.
Kocha Kovac akasirishwa na penalti
Kocha wa Croatia Niko Kovac ambaye alikuwa na hasira amesema mwamuzi kutoka Japan aliyesimamia pambano hilo la jana alikuwa hayuko katika kiwango chake, baada ya kutoa penalti kwa Brazil ambayo imebishaniwa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo huo wa ufunguzi.
Interaktiver WM-Check 2014 Trainer Kroatien Kovac Kocha wa Croatia Nico Kovac

Croatia ambayo iko katika nafasi ya 18 ya orodha ya FIFA ya timu bora duniani , ilikuwa ikijaribu kuzuwia na kuwatuliza Brazil katika kipindi cha pili hadi pale refa Yuichi Nishimura alipoamua upigwe mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wa Brazil Fred kuanguka wakati akipambana na mlinzi wa Croatia Dejean Lovren.
"Iwapo kuna mtu ameona kuwa ile ilikuwa penalti, anyooshe mkono. Siwezi kunyoosha mkono. Sikuona penalti, amesema kocha Kovac.
Kabla ya mchezo huo shabiki huyu aliifagilia Brazil na kusema:
"Brazil ina nafasi nzuri sana. Kikosi chake ni kizuri sana, upande wa mashambulizi na ulinzi pia."
Jioni ya leo(13.06.2014) Simba wa nyika , Cameroon , wataingia uwanjani kupambana na Mexico katika mchezo mwingine wa kundi A, wakati mabingwa watetezi Uhispania inaanza kampeni ya kurelijesha taji hilo mjini Madrid kwa kupambana na Uholanzi katika mchezo wa kundi B.

BRAZILI YAONYESHA UMWAMBA KWA CROATIA

Brazil yaibana Croatia 3-1


Neymar alifunga mabao mawili Brazil iipoilaza Croatia 3-1

Wenyeji wa kombe la dunia Brazil walitoka nyuma na kuilaza Croatia mabao 3-1 katika mechi ya kufungua fainali ya dimba la mwaka huu iliyochezwa katika uwanja wa Sao Paolo (Arena de Sao Paulo).
Mechi hiyo ilikuwa ikitizamwa na mashabiki 65,000 uwanjani humo baada ya kushuhudia tafrija ya ufunguzi iliyotizamwa na watazamaji zaidi ya bilioni moja kupitia kwa runinga
Wenyeji Brazil walitazamiwa kufunga bao la kwanza mapema katika mechi hiyo lakini uwanjani mambo yalikuwa tofauti ,Marcelo alijifunga mwenyewe na kuiweka Croatia mbele baada ya dakika 11 pekee ya kipindi cha kwanza .
Wenyeji waliotamaushwa na bao hilo walikuwa na matumaini kuwa kiungo machachari anayechezea Barcelona ya Uhispania Neymar atawaongoza ''the samba boys'' kutwaa taji lao la sita la dunia nyumbani.
Na nyota huyo hakuboronga alitumia kila mbinu ikiwemo kumbo iliyompelekea kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano na refarii kutoka Japan Yuichi Nishimura.
Hata hivyo dakika chache tu baada ya kuonyeshwa kadi hiyo ya njano Neyma alijifurukuta na kuisawazishia Brazil katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 22 aliiweka Brazil Mbele zikiwa zimesalia dakika 19 mechi hiyo kukamilika baada ya refarii kutoka Japan
Nishimura kupiga kipenga na kuashiria penalti baada ya Dejan Lovren kuonekana kama aliyemtega Fred katika eneo la lango.
hata hivyo picha za runinga zilizorejelea mara kadhaa hazikuonesha kama Lovren alimgusa Fred.
Wachezaji wa Croatia walijaribu kumshawishi mjapan huyo kuwa haikuwa kweli fred alikuwa amejiangusha lakini maoni yao hayakusikika.
Cameroon kukabiliana na Mexico hapo kesho

Neymar kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo aliiweka Brazil mbele kufuatia mkwaju huo wa penalti.
Vijana wa Luiz Scolari hawakuwachia hapo waliendelea kushambulia lango la Croatia na juhudi zao zilizaa matunda katika kipindi cha ziada Oscar alipompata kipa wa croatia ameduwaa na kufutamatisha kichapo hicho kunako dakika ya 91 .
Kufuatia ushindi huo wenyeji hao sasa wamejikita katika nafasi ya kwanza katika kundi A wakiwa na alama tatu.
Cameroon na Mexico zinashikilia nafasi ya pili na tatu katika kundi hilo .
Timu hizo zitakabiliana hapo Kesho.