- Wazazi wengi hufadhaishwa na mwenendo wa watoto wao wa kudorora kimasomo shuleni bila kujua kwamba hii inachangiwa na namna walivyoanza kuwakuza tangu walipozaliwa.
Upo uhusiano mkubwa kati ya chakula atumiacho mtu kwenye enzi zake za utoto na ukuaji wake wa akili.
Uwezo wa akili wa mtoto hujidhihirishwa katika viwango vya kufikiria na kuchanganua mambo anapoanza kusoma darasani.
Hii inatokana na kanuni za kisayansi kwamba afya
bora tangu utotoni humjenga mtu kiakili na kimaumbile. Hii ni pamoja na
lishe bora na afya njema. Hata hivyo, wanasayansi wanasema lishe bora tu
haitoshi kwa sababu suala la mazingira nalo huchangia katika kumjenga
mtu.
Mazingira mabaya kiakili ni kama vile vita, malezi
mabaya ya kifamilia, kukulia katika makundi maalumu kama vile makambi
ya wakimbizi, vituo vya kulelea watoto yatima, elimu ya kiwango cha
chini darasani na mtoto kujiingiza katika makundi ya vijana watukutu.
Pamoja na hali hiyo, wataalamu hao wanaamini kuwa
matatizo ya mazingira yaweza kurekebishwa, lakini yale yanayotokana na
lishe duni yanazaa tatizo la kudumu kimaisha.
Vyakula vyenye lishe bora ni vile vyenye mchanganyiko wa vyakula kama vile wanga, mafuta, protini, vitamini na chumvi chumvi.
Utafiti uliofanyika nchini unaonyesha kuwa familia
maskini ndizo zinazoshindwa kupata vyakula bora. Katika uchunguzi huo
inabainishwa kuwa familia nyingi hushindwa kutumia protini kutokana na
gharama yake sokoni kuwa kubwa kama vile nyama, samaki na mazao ya jamii
ya kunde.
Ni kutokana na utafiti huo, kampuni ya mbegu
Tanzania, TANSEED iliamua kubuni mbegu za mahindi zenye kiwango kikubwa
cha protini. Mtafiti wa TANSEED, Isaka Mashauri anasema waliamua kubuni
mbegu hiyo kwa zao la mahindi kwa sababu ndilo linalolimwa kwa wingi
zaidi nchini.
“Kilimo cha mahindi ni asilimia 80 ya mazao
mengine ya chakula. Hili hutumika kwa wingi zaidi na hupatikana kirahisi
zaidi,” anasema Mashauri ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa TANSEED.
Anasema aina hiyo ya mbegu ya mahindi waliyoipa jina TAN H611, tayari imeanza kusambazwa nchini.
Namna yalivyotengenezwa
Mashauri anatetea aina hii ya mahindi haikutokana na teknolojia ya Uhandisi Jeni, GMO.
No comments:
Post a Comment