ZIJUE AJALI MBAYA ZAIDI ZA
NDEGE KUWAHI KUTOKEA DUNIANI
TAREHE 3/3/1974- Watu 346
walifarii dunia katika ajali ya ndege ya Turkish Airlines DC-10 daaba ya kupata
hitilafu ghafla muda mfupi baada ya kuruka kutoka Paris Ufaransa, na kuanguka kwenye eneo la wazi
la Ermeonville nchini Ufaransa
Tarehe 27/3/1977-Ndege ya KLM
Boeing 747 wakati ikianza kukusanya kasi ya kuruka, iliigonga ndege nyingine ya
Pan American World Airways Boeing 747 wakati huo ikiwa kwenye njia ya kurukia, kwenye uwanja
wa ndege wa Los Rodeos huko Tanerife visiwa vya Canary na kusababisha vifo vya
watu 574 waliokuwemo ndani ya ndege hizo mbili.
Tarehe 25/5/1979-Bawa la
kushoto la ndege ya shirika la ndege la American Airlines DC-10 lilikatika na
kuanguka wakati ndege hiyo ikijiandaa kuruka kutoka uwanja wa ndege wa
kimataifa wa O’Hare, huko Chicago
nchini Marekani na kupelekea taharuki iliyosababisha vifo vyawatu 275 waliokuwa
ndani ya ndege hiyo na watatu waliokuwa ardhini.
Tarehe 28/11/1979-Kiasi cha
watu 275 walipoteza maisha wakati ndege ya shirika la ndege la New Zealand,
DC-10 baada ya kugonga mlima Erbus huko Antactica.
Tarehe 12/8/1985-Ajali mbaya
zaidi kuwahi kutokea kwa karibu miaka 30 iliyopita na kuhusisha ndege moja tu
ya abiria ni ile iliyotokea kwenye milima ya Japan ya kati ambapo jumla ya watu
520 waliuawa wakati ndege ya shirika la ndege ya Japan Airlines chapa namba 127
Boeing 747 ilianguka muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa
Tokyo, Lakini kwa miujiza ya Mungu, watu wane walinusurika.
Tarehe 26/5/1991-Dakika 12
baada ya kuruka, ndege ya shirika la ndege ya Lauda Air chapa namba 004 aina ya
Boeing 767 ilisimama ghafla angani na kasha kuanguka kiasi cha maili 70 kusini
Magharibi mwa Thailand ambapo watu 223 waliuawa pamoja na wahudumu wa ndege
hiyo.
Tarehe 11/7/1991-Breki ya
kutua ya ndege ya shirika la ndege ya Nigeria
DC-8 ilishika moto baada ya muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege
wa Jeddah, Saudi Arabia na ilishindwa kurudi
uwanja wa ndege na kuangukia pua kutoka umbali wa futi 10,000 ambapo jumla ya
watu 261 waliokuwa ndani ya ndege waliuawa.
Tarehe 26/4/1994-
Rubani wa ndege ya Shirika
la ndege la China, chapa namba 140, alimtaarifu muongoza ndege wa uwanja wa
ndege wa Nagoya nchini Japan, nia yake ya kutotua na kujaribu njia nyingine. Lakini
mambo yalikwenda kombo na muda mfuoi tu baadaye ndege hiyo aina ya Airbus A300
ilianguka wakati ikitua na kupelekea vifo vya watu 264 ambapo pia palipatikana
manusura wachache.
Tarehe 17/7/1996-Ndege TWA
namba 800 ililipuka angani muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa
kimataifa wa John F. Kennedy mjini New
York na kuacha vipande vya ndege vikianguka kwenye
pwani ya visiwa vya Long, Abiria wote 230 walifariki dunia. Chanzo cha mlipuko
huo ni hitilafu za umeme, ambapo waya wa umeme ulisafirisha umeme hadi kwenye
tenki la mafuka na kutokea mlipuko
Tarehe 12/11, 1996-Ndege ya
shirika la ndege ya Saudi Arabia, Boeing 747 na ile ya Kazakhstan II-76
ziligongana juu ya uwanja wa ndege wa New Delhi, nchini India ambapo watu 349 waliokuwemo
ndani ya ndege hizo mbili walifariki dunia
Tarehe 6/8/1997-Ndege aina
ya Boeing 747 chapa namba 801 ya South Korea, ikiwa karibu kabisa na kumaliza
safari yake huko Guam, ilijikuta ikianguka kwenye msitu na watu 228 waliuawa
ingawa wengine 26 walinusurika.
Tarehe 26/9/1997-Ndege ya
shirika la ndege ya Indonesia
aina ya Airbus A300 ilianguka huko Buah Nabar Indonesia ambapo abiria 234
walipoteza maisha, chanzo cha ajali kikielezwa kuwa ni hitilafu za umeme.
Tarehe 16/2/1998-Ndege ya
shirika la ndege ya China,
mruko namba 676 ikiruka kwenye hali mbaya ya hewa na mvua na ukungu kutoka Indonesia kwenda Taiwan, aliomba sehemu nyingine ya
kutua, lakini wakati akijiandaa kurudi alikotoka, ndege hiyo ilianguka maeneo
ya jirani ambapo watu 196 waliokuwa ndani ya ndege waliuawa na wengine saba
ardhini.
Tarehe 2/9/1998-Ndege ya
shirika la ndege ya Swiss ambayo iliondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa John
F. Kennedy mjini New York ikielekea Geneva Uswiss, ilianguka pwani ya Nova
Scotia, huko Canada
na abiria wote 229 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo MD-11 chapa 111, ilianguka
baada ya kupoteza umeme kwenye ndege nzima.
Tarehe 12/11-2001
Wiki chache baada ya
shambulio la kigaidi la Septemba 11 huko Marekani, ndege ya shirika la ndege ya
American Airlines, ilisababisha taharuki na hofu kubwa wakati ilipoanguka
kwenye bandari ya Belle huko Queen, jumla ya abiria 260 waliokuwemo
kwenye ndege hiyo aina ya Airbus A300 waliuawa na watu wengine watano waliokuwa
ardhini pia waliauawa
Tarehe 25/5/2002- Dakika 20
baada ya kuruka, ndege aina ya Boeing 747 ya shirika la ndege la China ilijibamiza kwenye Mkondo wa Taiwan
na kusababisha vifo vya watu 225
Tarehe 1/6/2009
Ndege ya shirika la ndege la
Ufaransa chapa 447 ikitoka Rio de Jeniero nchini Brazil, ikielekea Paris
Ufaransa, ilipotea wakati ikiwa inakatisha bahari ya Atlantic na baada ya siku
tano baadaye, miili ya kwanza ya watu ilionekana kiasi cha maili 600kwenye
pwani ya Kaskazini ya Brazil. Watu 228 walipoteza maisha
|
No comments:
Post a Comment