Kijiji cha Qunu chamuaga Mandela
Kijiji cha Qunu ambako atazikwa
Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika
kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.Ni viwanja hivi ambapo Madiba alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni na matunda ya misitu ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5, Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka 1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona tangu alipokuwa mtoto.
Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo, wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu nyumbani.
Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa pamoja na shule, alilemaji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo hili kutokana na makavazi aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.
Kuzikwa kwa Madiba
Ng’ombe dume atachinjwa, na jeneza la hayati Mandela kufungwa kwa ngozi ya Chui huku mzee mmoja wa familia akiongea na mizimu ya mfu hadi Madiba atakapozikwa.
Mazishi ya Mandela pia yatajumuisha tamaduni za watu wa jamii ya Xhosa ambako ukoo wa Mandela wa Thembu unatoka.
Bila shaka mazishi ya Mandela katika kijiji cha Qunu yatakuwa mchanganyiko wa mila na tamaduni , dini ya kikristo na pia watakaofika kutoa mazishi ya kitaifa.
Watu wa jamii ya Xhosa ambao ni moja ya kabila kubwa zaidi Afrika Kusini ikiwa na watu milioni saba wanatoka Kusini Mashariki mwa nchi katika mkoa wa Cape Mashariki.
Watu wa kabila la Xhosa wanatambua mizimu ya mababu zao na wao huzungumza nayo wakati wakitaka msaada.
Wanaamini kuwa lazima mwili ujulishwe kinachofanyika kabla ya kuuzika
Wanasema kuwa Madiba Lazima afahamishwe Jumapili kuwa anazikwa .
Lazima jeneza lake litafungwa kwa ngozi ya Chui kwa sababu alikuwa mtoto wa mfalme wa kitamaduni.
Lakini kwa sababu Madiba alikuwa Rais wa zamani , lazima pawepo bendera ya nchi. Bila shaka hii ni ishara ya heshima kwa kiongozi mheshimiwa.
Ng’ombe atachinjwa mapema alfajiri na kuliwa na watu waliofika kwa maombolezi. Na baada ya mwaka mmoja tangu kuzikwa kwa Madiba, Ng’ombe mwingine atachinjwa na kuliwa na familia ishara kuwa maombolezi yamekwisha.
No comments:
Post a Comment