Wednesday, May 14, 2014

UTURUKI YAPIGWA NA TETEMEKO



Kijiji cha Tabanli, Uturuki, baada ya tetemeko

Tetemeko kubwa la ardhi limetokea mashariki mwa Uturuki na kuangamiza majengo kadha.
Taarifa kamili hazijulikani, lakini meya mmoja wa eneo hilo alisema watu kadha walikufa.
Kitovu cha tetemeko hilo ni kijiji karibu na mji wa Van.
Naibu waziri mkuu, Besir Atalay, alieleza kuwa majengo 10 ya mji huo yameporomoka, na mengine 30 katika maeneo jirani.
Picha za televisheni zinaonesha watu wakichimba kifusi, wakitumia beleshi na mikono.
Taasisi ya Uturuki inayopima mitetemeko, inakisia idadi ya watu waliokufa inaweza kufika mamia kadha.

No comments:

Post a Comment