Friday, May 23, 2014

URUSI NA CHINA ZAIKINGIA KIFUA SYRIA

Urusi,China zapinga hatua dhidi ya Syria

Urusi na China zimepiga kura ya turufu kupinga uamuzi dhidi ya Syria
 Uchina na Urusi zimepigia kura ya turufu, kuzuia jaribio la baraza la usalama, la kutaka kuifikisha Syria katika mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC, kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Hili ni azimio la nne dhidi ya Syria, ambalo nchi hizi mbili zimelizuia.
Azimio hilo lingezielekeza Serikali na vikosi vya waasi nchini Syria katika mahakam hiyo ili zichunguzwe kutokana na ushahidi uliokusanywa na tume moja ya haki za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.
Ufaransa ilitoa rasimu ya azimio hilo baada ya kushindwa kwa mchakato wa kisiasa ulioidhinishwa na Umoja wa Mataifa na pia wakati kukiendela kushuhudiwa maovu yanayotekelezwa na pande zote mbili, ingawa zaidi na serikali.
Balozi wa Ufaransa alisema kuwa maadili yanapaswa kutumika kukabiliana na migawanyiko ya muda mrefu kuhusu Syria katika baraza hilo.
Lakini Urusi tayari imetangaza kwamba hatua hiyo ni ya kutafuta umaarifu na kwamba itaharibu jitihada za kutafuta amani na kwa pamoja na China ikapiga kura hiyo ya turufu kulipinga azimio hilo.

No comments:

Post a Comment