Wapatanishi kutoka kanda ya
Afrika Mashariki, wanafanya mazungumzo na wanasiasa kadhaa wa Sudan
Kusini walioachiliwa kujaribu kuhakikisha kuwa mkataba wa amani uliotiwa
saini Ijumaa unatekelezwa ipasavyo.
Wanasiasa hao ni pamoja na katibu mkuu wa chama
tawala Pagan Amum,aliyemsihi Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek
Machar kutekeleza mkataba huo na kuruhusu msaada kuwafikia waathiriwa wa
vita nchini humo.Tangu hapo maelfu ya watu wameuawa na wengine karibu nusu milioni kuachwa bila makao.
''Pande husika katika mgogoro huu lazima wazungumze na kuhakikisha wanamaliza vita,'' alisema Seyoum Mesfin, mkuu wa kikundi cha wapatanishi kutoka shirika la IGAD.
Vita vilizuka Jumapili baada ya mkataba kutiwa saini Jumamosi kati ya Rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha miezi mitano mkataba wa amani kupuuzwa.
Pande zote zinalaumiana kwa kufanya mashambulizi ardhini huku jeshi likisema kuwa siku ya Jumanne waasi walishambulia eneo wanalodhibiti la Dolieb, Kusini mwa mji unaokumbwa na vita wa Malakal.
Hata hivyo msemaji wa jeshi Kanali Philip Aguer aliambia shirika la habari la AFP, kuwa wanajeshi wanadhibiti maeneo yao wala sio kushambulia waasi.
No comments:
Post a Comment