Aliyezaa mtoto wa ajabu Handeni alonga
- Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri mkubwa kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri wamekuwa wakizaa katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika umri huo.
Tangu mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa
na wanawake walio juu ya umri wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo
waliotokana na teknolojia ya upandikizaji.
Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri
mkubwa kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri
wamekuwa wakizaa katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga,
Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika
umri huo.
Lakini Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na
wanawake wengi wanaozaa katika umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na
si kwa teknolojia ya upandikizaji.
Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13.
Daktari anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi
anasimulia mkasa wa mwanamke huyo akisema pamoja na umri, kingine
kilichomshangaza ni mtoto wa ajabu aliyemzaa .
Anaeleza kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi
wa Kata ya Sindeni zaidi ya mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito,
lakini walishangazwa na tumbo la mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana
kiasi cha kuhisi kulikuwa na tatizo fulani. Ndipo walipoamua kuanza
kumfanyia uchunguzi.
Baada ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine ya ultra sound
(kamera ya mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo
yasiyoeleweka hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa
Tanga, Bombo lakini walishindwa kutokana na hali yake.
Anasema baada ya kugundua kuwa hawataweza
kumsafirisha kutokana na hali yake, ilibidi wamuweke katika ulisimamizi
maalumu hadi siku ya kujifungua. Alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Katika upasuaji, madaktari walimtoa mtoto wa kwanza mwenye umbo la ajabu akiwa na kilo sita na wa pili akiwa na kilo 1.5.
Anafafanua kuwa mtoto alipotolewa tumboni ingawa
hakuwa wa kawaida, alikuwa anapumua. Baada ya muda alianza kutoka maji
na saa moja baadaye alifariki dunia. Mtoto mwingine aliishi kwa siku
moja na akafariki.
“Alikuwa na kilo sita pia alikuwa amevimba sana.
Huu ni uzito mkubwa sana kwa mtoto. Baada ya muda mfupi alianza kutoka
maji hadi mwili ukapungua kiasi na baadaye alifariki. Mwenzie aliendelea
kuishi kwa saa 24,” anasema Dk Mushi.
Mtoto huyo alizaliwa akiwa na miguu yote miwili,
lakini iliyoungana na kichwa chenye mdomo na masikio yanayoonekana kwa
mbali. Hana kiuno wala mikono.
No comments:
Post a Comment